Mwandishi wetu.
Taasisi ya uhifadhi na Utalii ya friedkin Conservation
Fund,imetoa msaada ya sh 110 million ili kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari
ya vipaji maalum mkoa wa Simiyu.
Msaada huo,ulikabidhiwa Jana kwa mkuu wa mkoa wa Simiyu
Anthony Mtaka na wakurugenzi wa taasisi
hiyo wakiongozwa na Abdukadir Mohamed katika hafla iliyofanyika uwanja wa
Maonesho ya Nanenane Nyakabindi wilaya ya Bariadi.
Mohammad alisema
Taasisi yao ambayo inamiliki kampuni za Uwindaji na upigaji picha za Kitalii,Mwiba holdings Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris, ambazo
zimewekeza mkoani humo,zimetoa msaada huo kusaidia watoto kupata elimu.
Alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ya kusaidia
jamii inayotolewa ili kuchangia maendeleo
ya mkoa wa Simiyu.
"Tunachoomba ni kupewa ushirikiano tufanye kazi
zetu za utalii katika pori la akiba la Makao na Maswa na kuondolewa uvamizi
" alisema
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Anthony Mtaka alishukuru msaada huo wa sh 110 milioni ambazo zitasaidia
ujenzi wa shule hiyo.
Alisema Taasisi ya Friedkin imekuwa na mchango mkubwa wa
maendeleo katika mkoa huo kwani hivi
karibuni ilitoa msaada ya mifuko 3000 ya saruji na bati 1000 kusaidia elimu.
Alisema licha ya msaada huo,taasisi hiyo imesaidia kutoa
ajira,inalipa kodi na imekuwa ikilipa kodi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Meatu Dk Joseph
Chilongani alisema serikali inatambua mchango wa taasisi hiyo kwa
maendeleo ya jamii.
Alisema licha ya misaada
inayotolewa ngazi ya mkoa Taasisi hiyo kila mwaka inatoa zaidi ya sh 610
milioni kama kodi ya pango na sehemu ya mapato ya utalii kwa vijiji 10
vilivyopo eneo la hifadhi ya jamii ya makao.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM(NEC) mkoa wa Simiyu
Gungu Silanga alisema serikali ya CCM itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo
kwani inachangia utekelezwaji wa Ilani ya uchaguzi.
"Miaka ya nyuma kulikuwa na watu wachache walitaka
kutogombanisha lakini sasa chama na serikali tupo pamoja kufanya kazi na
wawekezaji mkoa wa Simiyu.
Taasisi ya Friedkin conservation Fund yatoa sh 110 milioni kusaidia elimu Simiyu.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment