Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe
amesema kampuni zinazotoa huduma za ving’amuzi zinapaswa kuwarejeshea fedha wateja wanaotumia ving’amuzi
hivyo kutokana na kukiuka masharti ya leseni
Kamwelwe amezitaja kampuni hizo kuwa Azam, Dstv na Zuku na
kwamba zimekiuka masharti ya leseni zao
Kampuni hizo ziliondoa chaneli za ndani zisizolipiwa baada
ya tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), lililokusudia
kusimamisha leseni kwa maelezo ya ukiukwaji wa masharti
Tangazo hilo la TCRA lilieleza kuwa kampuni hizo zimekuwa
zikionyesha chaneli zilizopo kwenye orodha ya zile za bure kinyume cha matakwa
ya leseni zao ambazo zinaelekeza kuwa wasionyeshe
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Agosti 11,
2018 Kamwelwe amesema, “lazima watumiaji walipwe kwa sababu kampuni hizi zina
makosa na fedha hizo hazijalipwa serikalini. Subiri tutatoa deadline (muda wa
ukomo) wa namna watakavyolipwa watumiaji hawa wa ving’amuzi
Waziri Kamwelwe ameongeza akisema, “naona mmetuwahi
kutuuliza jambo hili, lakini niwahakikishe TCRA inalifanyika kazi kuhusu
urejeshaji huu. Lazima warudishe (fedha) kwa mujibu wa taratibu kwa sababu
wamefanya makosa.”
Amesema televisheni za ITV, Clouds, EATV na Channel Ten
walitoa maoni kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kadhia hiyo wakiwa na hoja kuwa
busara iliyotumika huko nyuma kwa vituo hivyo kupeleka maudhui yao kupitia
ving’amuzi vya Azam, Dstv na Zuku iendelee wakati utaratibu wa kurekebisha
sheria ukiendelea
“Jambo la msingi la kujiuliza ni TCRA kuendelea kuangalia
sheria na kanuni za utangazaji zikivunjwa kila kukicha au wachukue hatua ili
sekta ya habari iendeshwe kwa mujibu wa sheria?” amehoji Kamwelwe
Amesema kuna mambo mengi ya kujiuliza, baada ya uamuzi
uliolekeza utaratibu mpya wa matumizi ya ving’amuzi kama kanuni zinavyoelekeza
kwa watoa huduma wa Azam, DSTV na Zuku ambao walikwenda Mahakama Kuu kupinga
uamuzi wa TCRA, lakini shauri lao lilitupiliwa mbali Agosti 22, 2017
“Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali pingamizi hilo Agosti
22, mwaka jana. Baadaye watoa huduma hao walikwenda FCC kwa makundi mawili kwa
shauri hilo,” amesema Kamwelwe
Amefafanua kuwa kundi la kwanza lilihusu Azam ambalo
lilitupiliwa mbali na FCC na shauri la kundi la pili ni Azam, DSTV na Zuku
ambapo bado linashughulikiwa
“Kifungu cha 45 (5) cha Sheria ya TCRA ya mwaka 2003
kinasema kuwa uamuzi wowote wa TCRA katika kutekeleza majukumu yake ya
kudhibiti, utatekelezwa pasipo kujali iwapo mtu ambaye hajaridhishwa na uamuzi
amekata rufaa au anatarajia kuchukua hatua dhidi ya uamuzi huo,” amesema
“Hii ina maana watoa huduma hawa walipaswa kutekeleza uamuzi
wa TCRA kwanza pamoja na kuwa walikata rufaa FCC. Nitumie nafasi hii kuipongeza
Azam ambao wametekelezaagizo la Serikali.”
Kamwelwe ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuzingatia
kuwa ni lazima sheria na kanuni za nchi zifuatwe kikamilifu na kila mwenye
leseni aiheshimu
Pia, aliwataka wananchi kutumia ving’amuzi sahihi ili kupata
huduma za maudhui yasiyo na malipo
“Ving’amuzi vya Azam, Zuku na Multichoice havijazuiliwa,
bali vitaendelea kutumika kwa mujibu wa masharti ya leseni zao,” amesema waziri
huyo
Serikali yaagiza waliolipia ving’amuzi Azam, Dstv, Zuku warejeshewe fedha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 11, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment