Siku mbili baada ya kundi la wanaCCM kujitokeza hadharani
kupinga aliyekuwa mbunge wa Monduli, Julius Kalanga kurejeshwa kugombea ubunge
katika jimbo hilo, mwanasiasa huyo amechukua fomu ya kugombea akiwa mwanaCCM
pekee
Wiki mbili zilizopita, Kalanga alijiuzulu ubunge wa Monduli
aliokuwa akiushikilia kwa tiketi ya Chadema
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula
amekaririwa leo akisema kuwa, wanaompinga Kalanga wanaonyesha hofu tu, lakini
Kamati Kuu ya CCM ndiyo itakayoamua nani awe mgombea wao
katika kikao kitakachofanyika mwezi ujao
Leo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Monduli, Wilson Lengima
amesema hadi jana, siku ya mwisho ya kuchukua fomu za ubunge ni Kalanga pekee
aliyekuwa amechukua
"Taarifa nilizonazo ni kuwa amechukua fomu Kalanga
pekee na kama kutakuwa na mabadiliko tutatoa taarifa," amesema
Akizungumza Kalanga pia amesema amechukua fomu kutetea
wadhifa wake na kuwashukuru wanaCCM wenzake
"Nimechukua fomu za ubunge na nawashukuru sana wanaCCM
wenzangu kwa kuendelea kuniamini," amesema
Mapema wiki hii wanaCCM zaidi ya 40 kutoka kata tatu kati ya
20 za Wilaya ya Monduli waliandamana kumpinga
Kalanga kugombea ubunge kupitia chama na kutuhumu kuwapo kwa
njama za kutaka kumfanya mgombea pekee
Hata hivyo, hadi jana jioni ikiwa ni siku ya mwisho ya
kuchukua na kurejesha fomu ndani ya CCM, hakuna aliyempinga Kalanga
Kalanga mgombea pekee CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment