Wanafunzi wazuiwa kwenda shule baada ya mto kujaa maji


Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkoga, Kitongoji cha Tambani wilayani Mkuranga, Amiri Mbamba ameagiza wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaolazimika kuvuka Mto Kizinga, kutokwenda shule baada ya mto huo kujaa

Mbamba alitoa tangazo hilo jana jioni Mei 14, 2018 kwa kupita katika nyumba za eneo hilo na kuwasihi wazazi wasiwaruhusu watoto wao kutoka majumbani kwa ajili ya usalama wao

Mto Mzinga ulianza kujaa maji jana saa tatu asubuhi jambo lililowalazimu wavushaji eneo la Bonde la Mkoga kusitisha kazi hiyo

Hata hivyo, hali ya kujaa maji iliongezeka jana Jumatatu jioni na kusababisha sehemu ya daraja iliyokuwa ikitumika kufunikwa na maji hayo

Tangazo hilo pia liliwagusa wavushaji ambao wametakiwa kutovusha mwanafunzi yeyote hadi maji yatakapopungua

Watu wazima ambao walikuwa wanavuka kwenye mitumbwi walilazimika kulipa gharama ya Sh1,500 hadi Sh2,000

Wanafunzi wazuiwa kwenda shule baada ya mto kujaa maji Wanafunzi wazuiwa kwenda shule baada ya mto kujaa maji Reviewed by KUSAGANEWS on May 15, 2018 Rating: 5

No comments: