Wabunge CCM wapania kutoipitisha bajeti Wizara ya Kilimo 2018/19


Wabunge wa CCM, Richard Ndassa (Sumve) na Mashimba Ndaki (Maswa Magharibi) wamekataa kuunga mkono bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka 2018/19, kuwashawishi wabunge wenzao  wanaotoka maeneo yanayolima pamba, kutoipitisha bajeti hiyo hadi Serikali itakapoeleza sababu za bei ya zao hilo kushuka kutoka Sh1,200 hadi Sh1,100

Ndassa ndiye aliyeanza kuzungumza katika mjadala wa bajeti hiyo leo Mei 15, 2018 bungeni mjini Dodoma na kubainisha, “mheshimiwa mwenyekiti (Andrew Chenge) siungi mkono bajeti hii hadi nipate maelezo ya kutosha.”

“Pamba ni siasa na pamba ni uchumi na nisipopata maelezo ya kutosha siungi mkono bajeti hii. Waziri Mkuu alihamamasisha wakuu wa mikoa kumi na wilaya 46 zinazolima pamba walime nao wakalima.”

Amesisitiza, “Wananchi wakalima kweli kweli, lakini matarajio ya wakulima, kilo ilikuwa Sh1,200, lakini bila aibu bei ya sasa ni Sh1,100 hivi mkulima huyu tunamsaidia namna gani? Kila msimu unapoanza bei ya pamba peke yake, tatizo ni nini?”

Kwa upande wake Ndaki amesema bajeti hiyo hawawezi kuipitisha kama suala la ushirika halitafanyiwa kazi kwani linawakandamiza wakulima na kuwanufaisha wengine na kama hatutachukua hatua za haraka wakulima hawa hawatanufaika

Mara baada ya kauli hiyo ya ushirika kuwakandamiza wakulima, Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alisimama na kumpa  taarifa Ndaki kwamba baadhi ya vyama vya ushirika wamechagua viongozi wasio na sifa katika maeneno hayo, hawaaminiki.”
Kwa upande wake, Mbunge wa Mufindi Kaskazini (CCM), Mahmoud Mgimwa amesema kama Serikali haitatoa majibu kuhusu Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) atawahamisiha wabunge wote wanaotoka maeneo hayo kuikataa bajeti hiyo kama hawatapata majibu ya suala la ununuzi wa mahindi

Wabunge CCM wapania kutoipitisha bajeti Wizara ya Kilimo 2018/19 Wabunge CCM wapania kutoipitisha bajeti Wizara ya Kilimo 2018/19 Reviewed by KUSAGANEWS on May 15, 2018 Rating: 5

No comments: