Wabunge wahoji wakulima kuzuiwa kuuza mahindi nje ya nchi

Mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2018/19 umeendelea kuwa moto bungeni baada ya wabunge kuitaka Serikali kuacha kuwabana wakulima wa mahindi kuuza nje ya nchi.

Mbunge wa Kwela (CCM), Ignas Malocha akizungumza katika mjadala wa bajeti hiyo bungeni mjini Dodoma leo Mei 15, 2018 amesema, “Siungi mkono hoja, mkulima wa mahindi ni kama mfungwa, nilitarajia hotuba kama hii ingekuja na majibu lakini siyaoni.”

“Anauza gunia la mahindi Sh15,000, kitendo hiki hakiridhishi, hakifurahishi. Waziri (wa Kilimo Dk Charles Tizeba) anasema kuuza nje hadi apewe kibali apewe kibali, umelima wewee? Kama unaona ni shida yanunue uyahifadhi, si kazi ya mkulima kutunza. Si sahihi hata kidogo, nazungumza hili kwa niaba ya wananchi wangu zaidi ya laki nne, inawauma kweli kweli.”

Kuhusu kutotengwa kwa fedha za kilimo cha umwagiliaji, amesema: “Tuko makini  kweli katika kilimo, maendeleo ya viwanda duniani kote yalianza kwa mapinduzi ya kilimo, lakini kilimo kimewekwa pembeni, mtuulize sisi tunaoishi na wananchi.

 “Mimi nashangaa ndugu yangu Tizeba najua hii bajeti huiandai nyumbani kwako, hivi wataalamu wanafanya kazi gani kukusaidia. Hii  bajeti hupangi nyumbani kwako wanashauri kitu gani? hayo madigriii ya kazi gani kumuumiza mkulima.”

Mbunge wa Songea Mjini (CCM), Dk Damas Ndumbaro amesema, “Wananchi wa Songea wamenituma nifikishe ujumbe kwa wizara ya kilimo na Serikali. Wanasema kwao zao la mahindi ni chakula, kwao ni biashara na ni siasa, hawana viwanda, wanategemea mahindi, mahindi ndio uhai wao
“Lakini sasa hivi wana kilio kikubwa sana,  katika msimu uliopita mbolea haikupatikana kwa wakati, bei ya mbolea ilikuwa inabadilika kama homa ya vipindi, upatikanaji wa mbolea ulikuwa ni shida na ukiwanyima mbolea umewaua kabisa.”

Amesema wananchi wanajitahidi kuzalisha, akitolea mfano Ruvuma  mwaka 2016/17  walizalisha tani milioni 1.9, mahitaji na matumizi kwa mkoa mzima ni tani laki nne hivyo kulikuwa na ziada ya tani milioni 1.5


Wabunge wahoji wakulima kuzuiwa kuuza mahindi nje ya nchi Wabunge wahoji wakulima kuzuiwa kuuza mahindi nje ya nchi Reviewed by KUSAGANEWS on May 15, 2018 Rating: 5

No comments: