Mbunge wa Rombo (CHADEMA) Joseph
Selasini ameitaka serikali kutoa nafasi za ajira kwa vijana waliomaliza mafunzo
katika Jeshi la la kujenga Taifa (JKT) ili kuepuka hatari ya vijana hao
kujiingiza katika vitendo vya uhalifu baada ya kumaliza mafunzo.
Mbunge huyo amesema hayo Bungeni leo
Mei 14, 2018 wakati wa kuchangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Ulinzi na
Jeshi la kujenga Taifa na kuongeza kuwa serikali isipotoa ajira kwa vijana hao
itapelekea hali ya usalama wa taifa kuterereka kwasababu vijana hao wana
mafunzo kamili ya kijeshi.
“Kuna manung’uniko ya vijana kwamba
wale waliomaliza JKT awamu ya nne, hawajaajiliwa na hawanufaiki na utaratibu
huu, sasa hawa ni vijana ambao wamefunzwa siraha, wakiachwa na manung’uniko
mtaani tutakuja kutengeneza kitu kingine, hii inanipa hofu kama hatuwezi
kuajiri vijana wote ni vizuri tukaangalia vijana ambao tunaweza kuwapa mafunzo
ya kijeshi na wale ambao tunafikiria wataenda nyumbani wapewe mafunzo mengine,
vinginevyo kuwafundisha kijeshi na kuwaacha mtaani italeta athari kubwa sana”
amesema Selasini.
Mbunge huyo ameongeza kuwa wanajeshi
nchini wanapaswa kufanyiwa kipimo bora cha nidhamu yao kutokana na baadhi ya
uwepo wa baadhi ya wanajeshi kufanya matukio ya kiuhalifu katika makazi ya
wananchi.
Kwa upande mwingine Mbunge huyo
amesema kwamba serikali inatakiwa kuwekeza nguvu kubwa katika Jeshi ikiwemo
kutimiza mahitaji yote ya kifedha ili kuondoa fedheha ya jeshi kuwa na madeni
kutokana na upungufu wa fedha unalolikabili Jeshi hilo.
Bunge kwasasa linajadili mapitio ya
mapato na matumizi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa katika mwaka
wa fedha 2018/2019 ambapo Waziri Dkt Hussein Mwinyi ameliomba Bunge kuizinisha
kiasi cha shilingi trilioni 1.7 za wizara hiyo.
Vijana wapewe ajira jeshini - Mbunge Selasini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment