Serikali
imefuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini na wamiliki wake wametakiwa
kuomba upya wakizingatia Sheria ya Madini na kanuni zake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa
Mei 11, 2018 Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini, Profesa Idris Kikula
amesema tangazo la Serikali namba moja la mwaka 2018 limesema maeneo yote
yaliyopewa leseni yanarejeshwa serikalini bila hakikisho la kupewa tena
Amesema uamuzi
huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2019 ikisomwa na
marekebisho yake ya mwaka 2017 na kanuni ya 21 ya kanuni za Madini (Haki Madini
za mwaka huu).
Amesema leseni
zilizofutwa na wamiliki wake wanatakiwa kuomba tena zinazihusu kampuni 11,
kwamba leseni hizo zinajumuisha migodi ya kati na mikubwa
Migodi hiyo ni
pamoja na Kabanga Nickel Company Limited, National,Mineral Development
Corporation Limited, Bafex Tanzania Limited ambayo inamiliki leseni za maeneo
matatu
Nyingine ni
Mabangu Mining Limited, Resolute (Tanzania) Limited, Wigu Hill Mining
Company Limited, Nachingwea Nickel Limited na Precious Metals Refinery Company
Limited.
Serikali yafuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment