Mambosasa ampongeza Mange Kimambi

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amempongeza Mtanzania anayeishi Marekani, Mange Kimambi kwa maelezo kuwa ameipongeza Serikali

Mambosasa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Mei 11, 2018 katika mkutano wake wa waandishi wa habari na kumpongeza Mange ambaye alikuwa kinara wa kushawishi watu kuandamana Aprili 26, 2018 katika maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Kamanda huyo amesema Watanzania wanatakiwa kufika mahali wachague watu wa kuwashabikia

"Aprili 26 wananchi wa kanda yangu walipuuza uhamasishaji wake katika mitandao ya kijamii, sasa Mange huyo huyo anaipongeza Serikali,” amesema

Amesema kwa kuwa ameipongeza Serikali nao wanampongeza kwa kuwa sasa amerudi kundini

"Nampongeza kwa kuwa amerudi kundini alikuwa anapotosha na Watanzania walipopuuza na yeye ameamua kurudi na kuipongeza Serikali,” amesema Mambosasa

Kuhusu watuhumiwa waliokamatwa wakihusishwa na maandamano ya Aprili 26, Mambosasa amesema walioshukiwa kufanya walihojiwa na kupata dhamana.

Mambosasa ampongeza Mange Kimambi Mambosasa ampongeza Mange Kimambi Reviewed by KUSAGANEWS on May 11, 2018 Rating: 5

No comments: