Muigizaji na mchekeshaji maarufu
bongo Steven Nyerere, amesema anatamani kukutana na Rais Magufuli ili amshauri
azime data, ili watu wasitumie mitandao ya kijamii kwa kufanya umbea na kuongea
habari za uongo za kuchafuana.
Akizungumza Steve Nyerere amesema
iwapo atapata fursa hiyo atamsahuri Rais Magufuli kufuata wanachokifanya China,
ambapo wao wamepiga marufuku utumiaji wa mitandao ya kijamii mbali mbali, na
kutumia mitandao mingine ya kwao kwa ajili ya kukuza uchumi wao na sio kwa
ajili ya kupiga umbea na kueneza habari za uongo.
“Bado tunahitaji kuwa na mwenendo wa
China, nitafurahi sana siku Magufuli akizima data, na nadhani kuna haja ya
kumshauri Mheshimiwa Rais, kwa sababu kama tunataka kujenga Tanzania ya viwanda,
ni lazima siku moja tuzime data hata mwezi nadhani tutafikia malengo, tena
andika kabisa Nyerere anatamani kuonana na Magufuli amnong'oneze kuhusu data,
azime tu hata nwezi, ili watu wafanye kazi, amesema Steve Nyerere.
Steve ameendelea kwa kusema kwamba
….. “asilimia 90 wanaishi kwenye mitandao na kubuni vitu ambavyo haviingizi
taifa hata pato, nia ni kuliongezea taifa pato, wenzetu China wameendelea
kutokana kutoipa nafasi mitandao kuihairbu China yao, wameipa nafasi kwa ajili
ya kutangaza biashara na utalii, sasa sisi tumeipa nafasi kwa jili ya umbea”,.
Steve Nyerere ametoa kauli hizo zote
kutokana na watu kuzusha taarifa kuwa mke wake amemkimbia, baada ya kugundua
amezaa nje ya ndoa na muigizaji Welu Sengo.
Maisha ya Mtu
yako kwenye sura siyo kwenye akili
Natamani Magufuli azime data - Nyerere
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment