Ofisa habari
wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), Hellen Mtui
ameeleza namna walivyobaini kuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni hapo,
Edward Kahitwa amefariki dunia
Kahitwa
aliyekuwa akisoma shahada ya famasia chuoni hapo, mwili wake uligundulika Mei
19 katika chumba namba 65 kilichopo Hosteli ya Kagera alikokuwa akiishi peke
yake
Hellen alisema
jana kuwa kwa takriban siku tatu, wahudumu wa usafi waligonga mlango wa chumba
ili wafanye usafi lakini hawakufunguliwa
Alisema hali
hiyo haikuwa ya kawaida kwa wahudumu hao kutofunguliwa mlango na pia kulikuwa
na harufu iliyokuwa ikitoka ndani
Ofisa huyo
alisema wahudumu hao waliingiwa hofu na hivyo kwenda kuwaita walinzi walioamua
kuvunja mlango. Baada ya mlango kuvunjwa, walikuta mwili wa Kahitwa ukiwa
kitandani na baada ya hapo walitoa taarifa polisi
Alisema askari
walifika na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi
“Kahitwa ni
mtu wa Bukoba, lakini tumeambiwa ana ndugu yake Ununio, Dar es Salaam.
Tunatarajia kumuaga kesho (leo) asubuhi na baadaye mwili utasafirishwa kwenda
Bukoba ambako tunaambiwa ndiko mama yake yupo,” alisema Hellen
Chanzo cha
kifo cha mwanafunzi huyo bado hakijajulikana, polisi wakieleza kuwa wanaendelea
na uchunguzi
“Tumepokea
taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo lakini chanzo cha kifo chake bado
hakijafahamika. Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,”
alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni
Jitihada za
kuwapata wanafunzi wanaoishi jirani na chumba cha Kahitwa ziligonga mwamba jana
baada ya Rais wa Serikali ya wanafunzi Muhas (Muhasso), Geovanni Kihaga
kuwazuia waandishi wa habari akisema hawaruhusu mtu yeyote kuzungumzia suala
hilo
Alisema ibada
ya kuaga mwili wa marehemu itafanyika leo katika kanisa lililopo Muhimbili
“Tunapata
ugumu kulizungumzia suala hili kwa sababu kuna utata, wapo wanaosema marehemu
ni mtu wa Iringa, wengine wanasema Morogoro na wengine wanasema Bukoba. Familia
yake ndiyo itatupa mwongozo mzuri,”
Mwili wa mwanafunzi wa Muhas aliyefia chumbani ulivyobainika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment