Mwanaume wa miaka 47 alawiti watoto watatu mtwara


Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Mohamedi Kaisi Hamisi mwenye miaka 47 mkazi wa kijiji cha Kawawa mkoani Mtwara, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za ulawiti.

 

Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba mwanaume huyo anatuhumiwa kulawiti watoto watatu wenye miaka 13, 14 na 15, wa shule ya msingi Kawawa, walipokuwa wanatafuta Nazi kwenye minazi iliyopo vichakani baada ya kutoka

Kamanda Mkondya amesema kwamba baada ya kuwakuta watoto hao mtuhumiwa aliwatishia maisha kabla ya kufanya kitendo hicho cha kinyama katika eneo la Nambonde.

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwepo baada ya mtuhumiwa kukamatwa (Nassoro Abdala Nyoya, Sharifa Hassani na Julieta Athanas) kwa masikitiko makubwa wameiomba serikali ichukue hatua kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

Mwanaume wa miaka 47 alawiti watoto watatu mtwara Mwanaume wa miaka 47 alawiti watoto watatu mtwara Reviewed by KUSAGANEWS on May 23, 2018 Rating: 5

No comments: