Mbunge wa Geita Vijijini,
Joseph Musukuma Kasheku, amefungukia madai yaliyowahi kutolewa na Mbunge wa
Nzega Mjini Hussein Bashe, kwamba walitekwa na watu wa usalama wa Taifa ni ya
uongo na kwamba kilichotokea walikamatwa na askari na mbinu zilizotumika ni
zile wanazofundishwa bungeni.
Musukuma ametoa kauli hiyo wakati
alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara
kupitia ukurasa wa Facebook EATV kila Jumatano, ambapo amefafanua kwamba
walikuwa wakidhaniwa kufanya uhalifu.
Musukuma amesema kwamba "Mara
ya kwanza kulala polisi nimelala nikiwa mwana- CCM, mara ya kwanza Dodoma, mara
ya pili ni Geita, na nilikubali kwa sababu wala hatukutekwa, nilikuwa na kina
Bashe, nilimsikia rafiki yangu Hussein Bashe alisema tumetekwa, hatukutekwa".
"Tulikamatwa tukapelekwa polisi,
tukapekuliwa, tulipoonekana hatuna hatia tukaachiwa , hatukutekwa. Sikumjibu
Hussein Bashe aliposema tumetekwa kwa sababu sikuwepo, nasema hapa hatukutekwa,"
Musukuma.
Aprili 11, 2017 Mbunge wa Nzega
Mjini(CCM) Hussein Bashe aliwataka wabunge kuacha unafiki kuhusu Usalama
kuwateka watu na kwamba yeye ni mmoja wa watu waliokamatwa wakati wa mkutano
Mkuu wa CCM.
"Mimi nimekamatwa na
kuteswa na Usalama wa Taifa. Nimenyanyaswa sana nchi hii. Ikibidi mnifukuze CCM
- " alisema Bashe wakati Waziri wa Tamisemi,(kabla
hajaenguliwa katika nafasi hiyo) George Simbachawene kumtaka Mbunge wa Kigoma
Mjini, Zitto Kabwe kuthibitisha kuwa matukio ya ukamataji yanafanywa na usalama
wa Taifa.
Musukuma amkana Bashe kwenye kutekwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment