Watu
14 wamekamatwa wakihusishwa na mashambulizi hayo katika jimbo la mashariki mwa
India Jharkhand.
Polisi
wamesema wazee wa kijiji waliamuru wanaoshutumiwa kuhusika na ubakaji walipe
faini ya rupia 50,000 sawa na pauni 550 kama adhabu.
Watu
hao walighadhabishwa na maamuzi hayo na kuamua kuwapiga wazazi wa msichana huyo
kisha kumchoma moto binti yao.
''Watuhumiwa
wawili waliwapiga wazazi kisha wakakimbilia kwenye nyumba yao wakiwa na
washirika wao na kumchoma moto msichana'' Afisa wa Polisi Ashok Ram aliliambia
shirika la habari la Ufaransa.
Inaaminika
kuwa msichana huyo aliachwa nyumbani wazazi wake walipokwenda harusini.
Polisi wanasema
binti alibakwa na wanaume wawili katika eneo lenye msitu karibu na kijiji cha
Raja Kendua.
Baada
ya tukio hilo wazazi walikwenda kupeleka mashtaka kwa wazee wa kijiji
kuwashtaki wabakaji.
Mabaraza
ya kijiji hayana nguvu kubwa ya kisheria, hata hivyo yana ushawishi mkubwa
kwenye sehemu nyingi ya vijiji vya nchini India katika kusuluhisha migogoro
kuliko kutumia gharama nyingi kwenye mfumo wa mahakama.
Polisi
katika jimbo hilo wamesema wamewakamata watu 14 kati ya 18 ambao watachunguzwa
kutokana na madai ya ubakaji na uuaji.
mmoja
kati ya watu wawili waliotajwa kufanya shambulizi hajakamatwa, alieleza
Inspekta wa Polisi Shambhu Thakur alipozungumza na gazeti la Hindustan Times.
Hata
hivyo, wazee kadhaa wa vijiji wamekuwa wakishutumiwa kupitisha maamuzi kinyume
cha sheria na kuharibu ushahidi.
Tukio
hili limekuja wakati India ikikumbwa na matukio ya uhalifu wa kingono.
Takriban
matukio 40,000 ya ubakaji yameripotiwa nchini humo mwaka 2016.Matukio mengi
yamekuwa hayaripotiwi kwa sababu ya unyanyapaa.
Msichana wa miaka 16 achomwa moto kwa madai ya kubakwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment