Maelfu ya watu wameandamana jijini Paris nchini Ufaransa kupinga
mabadiliko yanayofanywa na serikali ya rais Emmnuel Macron.
Maandamano haya yamekuja wakati rais Macron mwenye miaka 40, akidhimisha
mwaka mmoja madarakani tangu kuchaguliwa kuwa rais wa taifa hilo la bara Ulaya.
Polisi wa kupambana na ghasia wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 2,000
walionekana jijini Paris, huku maandamano mengine yafanyika katika miji ya
Kusini ya Toulouse na Bordeaux .
Serikali imesema ililazimika kutuma maelfu ya polisi barabarani kwa hofu
ya kutokea kwa machafuko na uharibifu wa mali kama ilivyoshuhudiwa wakati wa
sikukuu ya wafanyikazi tarehe 1 mwezi huu.
Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa
ongezeko la maandamano nchini Ufaransa kupinga sera mpya za rais Macron
kwa watumishi wa umma ikiwemo sekta ya elimu na usafiri hasa wanaofanya katika
Shirika la reli.
Rais Macron ameendelea kusisitiza kuwa ataendelea na mabadiliko hayo, kwa
lengo la kuimarisha uchumi wa taifa hilo, licha ya pingamizi kutoka kwa
wafanyikazi wa umma.
Macron apingwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment