Mishahara mawaziri Malaysia yakatwa asilimia 10


Mawaziri walioteuliwa hivi karibuni katika baraza jipya wamekubali kukatwa asilimia 10 ya mishahara yao ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali ya Waziri Mkuu Mahathir Mohamad kubana matumizi
“Tuna wasiwasi kuhusu matatizo ya kifedha ya nchi. 

Tunajua kuwa mishahara ya mawaziri iko ya chini kuliko watumishi wa umma wa vyeo vya juu. (Lakini) sisi tutapunguza mishahara ya mawaziri kwa asilimia 10," Dk Mahathir aliuambia mkutano wa waandishi wa habari baada ya kuongoza mkutano wake wa kwanza wa Baraza la Mawaziri tangu kuwa waziri kwa mara ya pili
Deni la Taifa

Hatua hiyo imekuja wakati Serikali inahangaika kukabili deni la RM1 trilioni sawa na dola za Marekani 338.3 bilioni ambazo kiasi fulani kilikuwa kwa ajili ya miradi mikubwa

“Deni letu ni RM1 trilioni (fedha ya Malaysia inaitwa ringgit). Tunataka kutafuta mbinu ili tuweze kulipunguza. Tunataka kulikata lirudi chini,” alisema Dk Mahathir na akaongeza kuwa aliwahi kupunguza mishahara ya mawaziri siku za nyuma

Malaysia yashtushwa Deni la Taifa kufika RM1 trilioni

“Nilipochaguliwa kuwa Waziri Mkuu kwa mara ya kwanza mwaka 1981, jambo la kwanza kabisa nililofanya lilikuwa kukata mishahara ya mawaziri na watumishi wa umma

Alipoulizwa ikiwa pia atapunguza mishahara ya watumishi wa umma, alisema watumishi waandamizi wa umma wamekuwa wakilipwa mishahara minono kuliko mawaziri na hilo ni juu yao ikiwa wanataka kuchangia kupunguza gharama za uendeshaji wa nchi
Mishahara mawaziri Malaysia yakatwa asilimia 10 Mishahara mawaziri Malaysia yakatwa asilimia 10 Reviewed by KUSAGANEWS on May 25, 2018 Rating: 5

No comments: