Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, imepitisha
faini ya Sh300,000 kwa mfugaji atakayebainika kupitisha mifugo barabara kuu.
Akizungumza na kamati ya maendeleo ya kata za Lubili,
Sumbugu na Isenegeja wilayani hapa juzi, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,
Eliurd Mwaiteleke alisema faini hiyo itasaidia kupunguza uharibifu wa barabara
unaofanywa na wafugaji
“Barabara nyingi zimeharibika kwa sababu wafugaji wamekuwa
wanapitisha mifugo yao, hivyo niwaagize viongozi wote wa vijiji na vitongoji
kupitisha ushuru huo ili kukomesha vitendo hivyo,” alisema Mwaiteleke
Baadhi ya wananchi wa kata hizo mbali ya kukubali agizo la
mkurugenzi huyo, waliomba maofisa mifugo kuwaelekeza njia za asili
zitakazotumika. Ofisa mifugo na uvuvi wa halmashauri hiyo, Chrispin Shami
alisema kuna ng’ombe 160,996, mbuzi, 59,845 na kondoo 27,284 na kwamba
watahakikisha wanapitisha agizo hilo kuwa sheria ili watakaokiuka wachukuliwe
hatua
Alisema wanajitahidi kufufua majosho ya ng’ombe ili
kuwasaidia wafugaji kupeleka mifugo yao kupata chanjo
Katika tukio jingine, mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara,
Glorious Luoga amekutana na viongozi wa Kenya eneo la Maasai Mara kujadili
mgogoro wa wizi na uporaji wa mifugo uliofanywa eneo hilo na kijiji cha
Nyandage kata ya Nyanungu, wilayani Tarime
Uporaji huo unadaiwa kufanyika wakati wananchi kutoka Kenya
wakifuatilia mifugo iliyoibwa na nyayo kuonyesha kuingia nchini, wakiwa kijiji
cha Nyandage walimpora mtoto ng’ombe wanne kama fidia ya walioibwa. Kiongozi wa
ujumbe kutoka nchini Kenya, Anthony Mutuura alikemea kitendo hicho na kwamba,
kinaweza kuzorotesha uhusiano mzuri baina ya nchi hizi mbili
“Baada ya kuwahoji wakadai tunataka walete wetu nasi tuwape
wao kwa sababu nyayo zimeishia kwao,” alisema
Hata hivyo, Luoga aliwataka viongozi wa Maasai Mara kufika
kijiji cha Nyandage kupewa ng’ombe wao walioonekana kijijini hapo
Naye mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nyandage, Kemahi
Mirumbe alieleza kusikitishwa na uporaji ng’ombe uliofanywa akitaka utaratibu
kufuatwa
Ni takriban miaka 19 tangu wananchi wa nchi hizi mbili
waache kuibiana mifugo, baada ya kukomeshwa na Serikali mwaka ya 1999 Ngolo
John na Waitara Meng’anyi
Mifugo itakayo kanyaga lami faini Sh300,000
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment