MACHINGA ZAIDI YA 3000 WASAJILIWA NA KUTAMBULIWA RASMI


Wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga zaidi ya 3000 wamesajiliwa kwa ajili ya kupata vitambulisho vya kutambuliwa huku wafanyabiashara 100 wakisajiliwa na kupewa vitambulisho hivyo rasmi ikijumuisha kanda nzima ya kaskazini.

Akizungumza na wafanyabiashara hao mkuu wa wilaya ya Arushakwa niaba ya mkuu wa mkoa Fabian daqaro amesema serikali kwa kutambua umuhimu wa wafanyabiashara wadogo imeona ni vyema kutoa vitambulisho rasmi kupitia TRA lengo likiwa ni kuwatambua ili waweze kuwa uhuru bila kubughudhiwa na mtu yeyote ikiwa ni agizo la Raisi Dokta John Magufuli

Katika uzinduzi huo wa usajili wa utoaji wa vitambulisho wasio kwenye isiyo rasmi serikali imeona ni vema kuwapa wafanyabiashara hao kutambulishwa na kutimiza wajibu wao na kuchangia pato la taifa

Kwa upande wake kaimu kamsishna kutoka makao makuu TRA ndugu Zuberi Abdul amesma kuwa zoezi hilo ni la kitaifa na linafanyika nchi nzima kwa kutoa vitambulisho kwa wafanyabiashar ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa kuchangia pato la taifa kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania.

Hata hivyo amesema kuwa katika kutekeleza azma ya serikali mamlaka kwa kushirikana na wadau wengine ambao ni mamlaka ya vitambulisho NIDA serikali za mitaa wakala wa usajili ufilisi na Udhamini RITA pamoja na idara ya uhamiaji imeanza kutambua vikundi mbalimbali vya wafanyabiasharra kwa kuwapatia kitambulisho na namba ya kitambulisho cha mlipa kodi TIN

Hata hivyo ametoa rai kwa wafanyabiashara wote wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi kujiunga kwenye vikundi vinavyotambuliwa kisheria na serikali pamoja na usajili wa kurasimisha shughuli zao ili zitambulike serikalini na wadau wengine zikiwemo tasisi za fedha.

Kwa upande wa wafanyabiashara wamesema lengo la kuanzisha umoja wa vikundi ni ili kuomba srrikali iwapatie maeneo rasmi ya kufanyia biashara kwani wengi wao wamekuwa hawana maeneo rasmi


MACHINGA ZAIDI YA 3000 WASAJILIWA NA KUTAMBULIWA RASMI MACHINGA ZAIDI YA 3000 WASAJILIWA NA KUTAMBULIWA RASMI Reviewed by KUSAGANEWS on May 15, 2018 Rating: 5

No comments: