“MAAFISA HABARI WA MIKOA NA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUWENI WABUNIFU ILI KULETA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA HABARI KATIKA TAIFA LETU”
Na Fatuma S. Ibrahimu - Arusha
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo ambaye
pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dakta. Hassan Abbas alipokuwa akiwamegea Maafisa Habari wa Mkoa
pamoja na Jiji la Arusha siri kuu Nne
(4) za mafanikio katika kuleta mageuzi katika sekta ya Habari Serikalini.
Ameyasema hayo alipowatembelea Maafisa Habari wa Mkoa
pamoja na Jiji la Arusha mapema hapo jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Arusha ambapo lengo kuu la ziara hiyo ilikuwa ni kubaini changamoto mbalimbali zinazowakumba
maafisa habari hapa nchini.
Siri nyingine tatu ni pamoja na kuwa washauri na
wasemaji wakuu washughuli zinazofanyika katika maeneo yao ya kazi, kujali muda
pamoja na ushirikiano baina ya maafisa husika.
“Kada ya habari ni muhimili mkubwa wa taifa hili hivyo
wanahabari wote katika ngazi ya serikali mnapaswa kuisimamia kada hii kwa weledi na kujituma kwa hali na mali na mtambue
nafasi zenu zina mchango mkuwa kwa serikali katika kupeleka taarifa sahihi kwa wananchi”
alisema Dakta. Abbas.
Aliongeza kuwa, kada ya Habari Serikalini iwe chachu ya
kusaidia kutangaza na kutetea mageuzi mbalimbali yanayoendelea hapa nchini chini
ya serikali ya awamu ya Tano.
Katika zara yake hiyo Dakta. Abbas aliambatana na
uongozi mzima wa Chama
cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Serikali (TAGCO) ambapo mkakati huo
wa idara ya Habari Maelezo na Ofisi ya
Msemaji Mkuu wa Serikali ni endelevu katika Mikoa na Halmashauri zote hapa nchini.
MWISHO.
“MAAFISA HABARI WA MIKOA NA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUWENI WABUNIFU ILI KULETA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA HABARI KATIKA TAIFA LETU”
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment