Kamanda wa Polisi mkoa
wa Kipolisi Tarime/Rolya Henry Mwaibambe, amesema kwamba tuhuma zinazoenea
mitandaoni kuhusu tofauti iliyopo kati ya jeshi la Polisi na familia ya
marehemu Suguta aliyeuawa na polisi hadi kufikia kutaka kususa kuzika maiti,
sio za kweli kwani wana ushirikiano mzuri.
Akizungumza Kamanda Mwaibambe amesema kama
jeshi la polisi wametoa ushirikiano wao tangu tukio la mauaji lilipotokea kwa
kutoa taarifa kwa familia, kuelezea mazingira ya tukio, na kuwashirikisha hata
kwenye 'postmoterm', na hata baada ya kikao cha familia kupita, walishirikishwa.
"Hakuna mgogoro wowote, hakuna
fujo ya aina yoyote watu wametulia wanaendelea na shughuli zao, tuliwaambia
ukweli tukio limetokea, tukazungumza na wanafamilia, hata 'postmoterm'
tuliwaambia, na hata wao walipokaa kikao cha familia wakaamua kwamba tutauzika
mwili wa ndugu yetu kwa heshima zote na kila kitu tunashirikiana nao”, amesema
Kamanda Mwabambe
Sambamba na hilo Kamanda Mwaibambe
amesema alifuatilia kwa kina kujua nini chanzo cha skari huyo kumuua Chacha
Suguta, na kubaini ni mgogoro uiojitokeza baada ya kumwambia maneno yasiyofaa.
"Nimefuatilia kuna maneno
ambayo ya kilugha yalitamkwa kwa Kikurya ingawa siwezi kuyasema moja kwa
moja, ndio yalimsababisha yule askari apate jazba namna hii, ila yalikuwa
maneno yasiyofaa ”, amesema Kamanda Mwaibambe.
Chacha Suguta ambaye ni mdogo wa
Mbunge wa Tarime vijijini John Heche aliuawa kwa kuchomwa kisu na polsi
aliyemkamata, April 27, 2018.
Kamanda Mwaibambe afunguka kususiwa maiti
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment