Siri ya tukio la utekeji wa mwandishi wa habari jijini Arusha aliyetekwa na kudhalilishwa akiwa utupu,imefichuka baada ya jeshi LA Polisi Mkoani Hapa kumtia mbaroni Mrembo anayefanyakazi ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha ,ambaye ndio chanzo cha tukio hilo.
Mrembo huyo Amina Mshana au Loveless anayefanyakazi kitengo cha masijala,katika ofisi hiyo,anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumrubuni na kumteka mwandishi wa habari wa kujitegemea jijini hapa Lucas Myovera kwa madai ya kutaka amwandikie habari zake .
Loveness akiwa na mpenzi wa ,Swalehe Mwindadi anayefanyakazi ofisi ya Mkuu wa mkoa kama ofisa protocol, ambao wote wanashikiliwa na polisi,Mkoani hapa ,siku ya tukio aliendesha gari dogo aina ya Toyota IST Mali ya Mwindadi, lililotumika kumteka mwandishi huyo nakumpeleka kusikojulikana akiwa amefungwa kamba,miguuni na mikononi na kumdhalilisha.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ,Yusufu Ilembo amesema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Hata hivyo mapema Leo Amina na Swalehe waliokuwa wameachiwa kwa dhamana jana Mey 17 walikamatwa tena na kurejeshwa kituoni na leo Mey 18 walitolewa na kwenda kufanyiwa upekuzi nyumbani kwao.
Huyu Dada ni kati ya waliohusika kumteka mwandishi wa habari Arusha na kumdhalilisha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 18, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment