| Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara,Simon Lulu akipokea kadi ya Chama Cha ACT Wazalebdo kutoka kwa aliyekuwa diwani wa kata ya Gihandu,Mathayo Semuhenda. |
| Aliyekuwa diwani wa kata ya Gihandu kwa tiketi ya ACT Wazalendo,MATHAYO SEMUHENDA akipokea kadi ya CCM baada ya kutangaza azma yake ya kujiunga na CCM. |
| Aliyekuwa diwani wa kata ya Gihandu,Mathayo Semuhenda akila kiapo cha uadilifu mara baada ya kukabidhiwa kadi ya chama cha mapinduzi(ccm) |
ALIYEKUWA diwani wa kata ya Gihandu,wilayani Hanang,Mkoani Manyara kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo,Mathayo Samuhenda amejiuzulu udiwani wa kata hiyo na kujiunga na Chama Chama Mapinduzi (CCM)
Akitangaza azma yake hiyo ya
kujiuzulu katika nafasi yake ya udiwani wa kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Gihandu,Samuhenda alisisitiza
kwamba aliamua kujiuzulu na kuwaacha wapiga kura wake siyo kwa njia ya ukatili
bali alifikia maamuzi hayo kwa lengo la kuwaunganisha wananchi wote wa kata
hiyo.
Aidha alifafanua kwamba katika
kipindi cha zaidi ya miaka miwili sasa wananchi wa kata hiyo wana matatizo ya
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kutokana na wanasiasa kutumia
mtaji huo kuomba kura.
“Inatosha wanasiasa sisi tutumie
shida ya maji ili tuoate kura tuondoke,inatosha..na watu wa Gihandu nawaomba
sana hiyo ikiletwa kama sehemu ya mnada mzuri tu wa mtu kujinadi mkataeni
inatosha tumeumia vya kutosha.”alisisitiza Samuhenda.
Hata hivyo diwani huyo aliyejiuzulu
aliweka bayana kwamba umefika wakati sasa kwa wanasiasa kubadili ajenda za
kupatia kura za Gihandu na isiwe upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama
kwani hiyo sasa imekuwa ni kejeli
Akimpokea diwani huyo,Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Manyara,Simon Lulu alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa
wanaoendeleza makundi licha ya kuwa hivi sasa siyo wakati wa kumpeni na badala
yake aliwataka kuvunja makundi hayo na kusisitiza juu ya utekelezaji wa miradi
ya maendeleo kwenye maeneo yao.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo
alisisitiza pia kwamba suala la kuvunja makundi siyo la hiyari bali ni la
lazima kutokana na makundi hayo baadhi ya wanachama mchana wanakuwa CCM huku
usiku wanatumikia Vyama vya upinzani.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Hanang,Methew Darema alimpongeza diwani huyo kwa kitendo chake cha ujasiri cha
kujiuzulu nafasi aliyokuwa nayo pamoja na kwamba ni hivi karibuni alitembelewa
na kiongozi wake wa kitaifa kwa lengo la kuhamasisha watu kujiunga na chama
hicho.
Kwa upande wake baadhi ya wananchi
wa Kijiji cha Gihandu,Stephano Ngudu alisema mwaka 2008 kila mwananchi
alichangia shilingi 86,500/= kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari na
Hosteli mbili,lakini mpaka leo hakuna ujenzi wowote wa majengo hayo
uliokamilika na fedha walizochanga hawajarudishiwa.
ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU NA KUJIUNGA NA CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 02, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment