ZITO KABWE AMJIBU POLEPOLE KUWA YUKO TAYARI KUKAMATWA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole amedai kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe hajui hesabu kwa kuwa hakuna fedha iliyopotea hivyo amemshauri amtafute mtaalam wa hesabu

Polepole amesema hayo leo Jumatano Aprili 18 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG

Polepole amesema, “Huyu ni muongo alianza na santuri ya njaa akatangaza nchi ina njaa. Tumezunguka nchi nzima hakuna njaa, akaona haitoshi akamgeukia rais wetu kuwa ni dikteta wakati yeye anaendesha chama kupitia Facebook.”

“Kuna wakati anasema kamati kuu imekaa kumbe uongo anaandika facebook”

 “Niombe uongozi wa Bunge wakati mwingine uwe unawabana wabunge wawe wanathibitisha mambo wanayoyazungumza bungeni.”

“Wenye dhamana ya kusimamia sheria wachukue hatua, kucheka cheka na mizaha kwa kauli hizi haivumiliki. Tunataka aeleze hiyo Sh 1.5 trilioni kaipata wapi, alizua taharuki, nasisitiza tusimuache alizoeshwa vibaya huyu maana tunajua sisi ndio tupo kwenye chama.”

Baada ya Polepole kueleza hayo Zitto amejibu katika mitandao ya kijamii akieleza, “Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha kuhusu TZS 1.5trilioni zinazohojiwa na CAG”

“Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo (haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo).Chama cha Mapinduzi(CCM) kimesema kuwa kuna viongozi wa upinzani wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kuupotosha umma, tabia ambayo haikubaliki, haivumiliki na itafika wakati watasema sheria ichukue mkondo wake maana wanaleta taharuki kwa wananchi
ZITO KABWE AMJIBU POLEPOLE KUWA YUKO TAYARI KUKAMATWA ZITO KABWE AMJIBU POLEPOLE KUWA YUKO TAYARI KUKAMATWA Reviewed by KUSAGANEWS on April 18, 2018 Rating: 5

No comments: