Jeshi la Israel limewaua
Wapalestina 7 kwa kuwapiga risasi, na wengine 1,070 wamejeruhiwa, wakati wa
maandamano yaliyofanywa jana na maelfu ya Wapalestina karibu na mpaka wa ukanda
wa Gaza, huku wengi wakichoma matairi na kutupa mawe.
Baadhi ya vyombo vya
habari vimemnukuu balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa akisema idadi ya
waliouawa ni 9.
Kijana mwenye umri wa miaka 16 ni miongoni mwa waliouawa.
Aidha, mwanamke mmoja na
watoto ni kati ya wale waliojeruhiwa pamoja na waandishi wa habari wa
Palestina.
Tangu Ijumaa ya wiki
iliyopita, Wapalestina 29 wameuawakufuatia taharuki katika mpaka huo, na watu
2,500 wamejeruhiwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Antonio Guterres na viongozi wengine wametaka uchunguzi huru kufanywa
kuhusu mauaji hayo.
Maafisa wa Israel
wametetea hatua walizochukua kwa kusema baadhi ya Wapalestina waliouawa
waliwafyatulia risasi wanajeshi wake, na baadhi yao walikuwa wana mafungamano
na kundi la Hamas. Wapalestina hao wanafanya maandamano ya wiki sita kupinga
mzingiro wa mpakani ambao umedumu kwa muongo mmoja sasa.
Watu 7 wauawa na zaidi ya 1,000 wajeruhiwa .
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment