Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema anajua wapo
watakaotumika kuleta vikwazo kwenye hatua anazopiga za kuiletea maendeleo nchi.
“Katika
juhudi hizi za kuleta maendeleo wapo wengine watasaliti njiani, wapo wengine
watatumika na mbinu za mabeberu, na hasa katika masuala haya ya kujenga nchi
yetu, na hasa kwa sababu nchi yetu inakwenda mbele, ni lazima itawakwaza
wengine, katika jukumu lolote la kazi hata kwenye familia, lazima watapatikana
wa kupinga pinga kidogo, lakini kikubwa ni kunyoosha mstari kwa ajili ya
kuwatumikia Watanzania masikini”, amesema Rais Magufuli.
Sambamba na hilko Rais Magufuli amemuhakikishia mtoto wa Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere, Makongoro Nyerere, kuwa nchi ipo salama na imara, na anaamini itafika ikiwa imara zaidi licha ya vikwazo vingi anavyokutana navyo.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa jengo la PSPF mkoani Dodoma, Rais Magufuli amesema kwamba
wapo ambao hawapendi kuona Tanzania inapiga hatua kwenye uchumi, hivyo
watu watatumika na mabeberu kuleta vipingamizi na vikwazo, lakini yeye
ataendelea kuchapa kazi kwa ajili ya watanzania masikini.
Sambamba na hilko Rais Magufuli amemuhakikishia mtoto wa Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere, Makongoro Nyerere, kuwa nchi ipo salama na imara, na anaamini itafika ikiwa imara zaidi licha ya vikwazo vingi anavyokutana navyo.
Wapo watakaotumika na mabeberu – Rais Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment