Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda amegharamia gharama mbalimbali katika msiba wa Agnes Gerald alimaarufu
kama Masogange ambaye amefariki April 20, 2018 na kuzikwa leo April 23, 2018
jijini Mbeya.
Akiongea mbele ya waombolezaji na
Mkuu wa mkoa wa Mbeya mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Matebe Mathias 'MC
Pilipili' ambaye ndiye 'MC' wa shughuli za mazishi ya Agnes Masogange amesema
kuwa wameona mkono wa serikali katika hilo na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam ndiye aliyefanikisha na kulipia magari ambayo yamewapeleka wasanii
mbalimbali Mbeya.
"Mkuu wa mkoa wa Mbeya kuna
upendo mkubwa ambao tumeuona kutoka kwenu kwani ulikuwa karibu na sisi muda
mwingi, ulikuwa ukitupigia simu kujua tupo wapi hivyo naamini usiku wa leo
hujalala kabisaa.
"Pia tunamshukuru Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam kwani yeye ndiye aliyelipia magari mawili, matatu ambayo
yametuleta hapa Mbeya leo kutokea Dar es Salaam, hata kamati ambayo ilikuwa
imeandaa kuanzia kutoa heshima ya mwisho pale Leaders Club ambayo ilikuwa chini
ya Steve Nyerere ilipewa nguvu na watu wa serikali tumeona serikali mmetupa
support vizuri" alisema MC Pilipili
Mbali na hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Amos Makalla aliweza kuwapokea na kutoa neno la shukrani kwa wasanii na watu
mbalimbali ambao wameweka tofauti zao pembeni na kuungana kuwa kitu kimoja
katika kuhakikisha wanampumzisha salama mwenzao katika nyumba ya milele.
"Mueendelee kuwa pamoja hivi
hivi bila kujali tofauti zenu, mabifu yenu mzidi kuwa wamoja kwani hili jambo
mmejenga heshima kubwa sana, naomba nitoe pole sana kwa familia kwa msiba
huu" alisema Makalla
Makonda agharamia mazishi ya Agness Masogange
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment