Dar es Salaam. Mwanahabari
Mkongwe, Jenerali Ulimwengu amesema ukandamizwaji wa demokrasia nchini
unasababishwa na hofu ya wananchi kuwahoji viongozi wao, huku akitaka
kujengwa kwa jamii inayohoji tangu ngazi ya familia hadi Taifa
Ulimwengu ameyasema hayo leo
Aprili 13, katika mkutano wa 10 wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika
jana katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ulimwengu aliwataka wananchi
kutokubali mambo kirahisi bali wawe wadadisi
“Ndio maana tunatakiwa kuwauliza
wenye madaraka, kwa mtu anayeongoza, nani amekupa mamlaka ya kusema hakuna
maandamano ya kisiasa? Au unasema hakuna kufanya mkutano kwenye mkoa huu kwa
sababu huishi hapa?” Amehoji Ulimwengu
Ameongeza: “Nani aliyekwambia
kwamba tukishamaliza uchaguzi na ikiwa umeshinda hakutakuwa na kampeni za
siasa hadi uchaguzi mwingine ufike? Haya yote ni madaraka waliyojipa watu,
wamejilimbikizia na kwa sababu hatuulizi kikamilifu, wanafikiri wako sawa.”
Ulimwengu ametaka kujengwa kwa
jamii inayouliza maswali tangu ngazi ya familia na kuwataka wazazi kuwaruhusu
watoto kuwauliza maswali.
“Utamaduni wa kuhoji unaanzia
nyumbani, waacheni watoto wawaulize maswali na muwe tayari kuwasikiliza. Wale
wenye wajukuu nao waulize maswali. Kwa hiyo tuanzie kwenye nyumba zetu,
vijijini na mitaani, tujenge jamii ya watu wasiochukulia vitu kiurahisi, bali
wanauliza kila kitu,” amesema Ulimwengu
|
Ulimwengu: Demokrasia inaminywa kwa sababu watu hawahoji viongozi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment