Uchunguzi bado sakata la Mtanzania aliyeuawa Uingereza


Mwili wa Mtanzania, anayedaiwa kuuawa na mume wake, Uingereza Leyla Mtumwa, bado haujafika nchini kutokana na uchunguzi kutokamilika

Leyla, 36 anadaiwa kuchomwa visu shingoni na kifuani hadi kufa na mume wake, Salum Kasambula (38) usiku wa kuamkia Ijumaa Kuu, mwezi huu. Mauaji hayo yalifanyika nyumbani kwa wanandoa hao, Kirkstall Avenue, Haringey, Uingereza

Mama wa marehemu Hidaya Mtumwa ambaye amesema: “Mwili bado haujaletwa kwa kuwa uchunguzi haujakamilika mpaka sasa,” amesema mama yake Leyla, Hidaya Mtumwa

Hidaya pia amesema suala la fedha za kuuleta mwili nchini limekamilika lakini kinachosubiriwa ni uchunguzi tu
Hidaya ni yule mwanamke aliyewahi kutungiwa wimbo na mwanamuziki wa DR Congo, Pepe Kalle, miaka ya 90.

Uchunguzi bado sakata la Mtanzania aliyeuawa Uingereza Uchunguzi bado sakata la Mtanzania aliyeuawa Uingereza Reviewed by KUSAGANEWS on April 13, 2018 Rating: 5

No comments: