Serikali ya Uingereza imewataka wananchi
wake wanaoishi hapa nchini kuchukua tahadhari na maandamano ya kisiasa
yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya
habari leo Aprili 24 imesema kwamba kuna raia zaidi ya 75,000 wanaoingia nchini
hapa kila mwaka
Hivyo imewatahadharisha kujihusisha na
maandamano hayo kwa madai kwamba wanaweza kupata madhara kutoka kwa jeshi la
polisi
Katika taarifa hiyo ilitolewa tahadhari
kwamba kwa sababu
maandamano hayo yalishapigwa marufuku hivyo polisi ni lazima
watatumia mabomu ya machozi au silaha za moto
“Hivyo muwe makini sana mnapokuwa kwenye
mizunguko yenu muepuke mikusanyiko ya watu au watu wanaoandamana, muda wote
muwe mnasikiliza vyombo vya habari, mjue nini kinachoendelea,’’ ilisema taarifa
hiyo na kuongeza
“Ikiwa mnahitaji mawasiliano na namba ya dharura
ya kupiga haraka ni 112 uliza huduma ya dharura unayohitaji.’’
Pia taarifa hiyo iliwataka raia hao wa Uingereza kuwa makini wawapo barabarani kwa sababu watu wanaweza kutumia mwanya huo kufanya jambo lolote nchini hapa
Chanzo: mwananchi
UK yaonya raia wao kuhusu maandamano Aprili 26
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment