"Tunafanya makosa sana kudhani sisi wanasiasa ndiyo wenye dhamana ya amanii Kuliko Viongozi wa Dini " -John Kadutu
Mbunge wa Ulyankulu
(CCM), John Kadutu amesema wabunge na wanasiasa wengi wanafanya makosa kudhani
wao ndio wenye dhamana ya amani ya nchi kuliko viongozi wa dini na kudai kuwa
yeye yupo tayari kutofautiana na wanasiasa hao lakini anaamini 2020 watarudi
kutaka kuombewa tena na viongozi hao
Kadatu amesema hayo bungeni na kudai
kuwa viongozi na wanasiasa hao wanapooambiwa mambo fulani fulani huwa
wanafurahia sana lakini wakiguswa mambo yao wanabadilika na kuanza kuwabeza na
kuwaadaa viongozi wa dini.
"Suala la amani ndugu wabunge
si jambo la kikundi fulani wala si jambo la wabunge pekee yake bali dhamana ya
amani ya wananchi na watanzania wote tunafanya makosa sana kudhani sisi
wanasiasa ndiyo wenye dhamana ya amani, juzi niseme wazi mimi sikufurahishwa
kabisaa na mjadala wa kuwajadili viongozi wa dini sisi ni sehemu yake na wao ni
sehemu yetu kila wakati viongozi wa dini wanatuhubiri tuache mambo mabaya
mnaambiwa muache kuzini, muache wizi, muache rushwa mnashangilia lakini
mkiambiwa jambo linalogusa mambo yenu mengine mnakuja juu, tumerogwa na nani
watanzania kudhani kwamba viongozi wa dini wanachosema ni cha uongo, leo
unakwenda kanisani unanyenyekea unasali unanyenyekea leo ukiambiwa hili jambo
halifai unakuja juu, Watanzania tuache mambo haya" alisisitiza Kadutu
"Mbona sisi tukifanya haya
mambo humu bungeni tunapelekana kwenye Kamati ya Maadili, wapi sasa wao
watajadili kwani wao hawana Kamati ya Maadili wao kupitia majukwaa ya makanisa
na misikiti ndiyo uongozi tulionao na kila siku tukipata mafanikio tunakwenda kunyenyekea
kuombewa, hakuna mtu humu bungeni hajaombewa baada ya kupata ubunge hapa lakini
leo tunawabeza viongozi wetu wa dini na mimi nipo tayari kutoelewana na wengine
najua 2020 tutakutana huko tukiwaombeeni"
"Tunafanya makosa sana kudhani sisi wanasiasa ndiyo wenye dhamana ya amanii Kuliko Viongozi wa Dini " -John Kadutu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment