WAZIRI wa Uchukuzi James Macharia amesema kuwa nauli zinazotozwa
hasa na matatu Jijini Nairobi lazima zipungue kufuatia juhudi mpya za kutenga
barabara zitakatotumika na magari hayo pekee.
Waziri ambaye alikuwa mbele ya Kamati ya Seneti ya Barabara
alisema kuwa wanaanza majaribio ya mpango huo na barabara ya Thika
Superhighway, ambapo kutakuwa na barabara iliyotengewa magari ya uchukuzi wa
umma kutoka mtaa wa Githurai hadi katikati mwa jiji.
“Nauli zinastahili kupungua, lazima zipungue. Wachukuzi wa magari ya umma
wamekuwa wakisema kuwa nauli ziko juu kwa sababu ya muda mwingi wanaokaa kwa
msongamano barabarani. Tunaanza na njia ya moja kwa moja kutoka Githurai hadi
Katikati mwa Jiji katika barabara ya Thika.
Nauli inayotarajiwa kulipwa ni Sh40,” amesema Dkt Macharia.
Waziri ameeleza kuwa mbali na mabasi ya Huduma ya Vijana kwa Taifa
(NYS), Wamiliki wa Matatu pia wanatarajiwa kuleta nchini mabasi 50 ambayo
yatatumika kuimarisha usafiri jijini.
Wamiliki wa matatu wamepinga mpango wa serikali kuingilia biashara
hiyo wakihofia kuwa inalenga kuwasambaratisha.
Nauli
Macharia aliambia kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Kiambu, Bw
Kimani Wamatangi, kuwa ingawaje nauli humu nchini hazijadhibitiwa, mpango huo
wa kutenga barabara utasaidia katika kushauri kiasi cha nauli kinachofaa.
Wakati huo huo, waziri alieleza kuwa huduma hiyo inatoa suluhisho
la muda, kwa uchukuzi na sekta hiyo inawahitaji wawekezaji wa kibinafsi
kuhusika.
Pia alisema wanatarajia kuwa matatu za abiria 14 zitaondolewa
kabisa barabarani katika harakati za kuboresha uchukuzi jijini.
Jiji la Nairobi aliambia kamati hiyo linahitaji takriban mabasi
900 kuweza kuendesha vilivyo usafiri unaotegemewa, na ambao utakuwa na viwango
vinavyowavutia Wakenya wa ngazi zote.
SERIKALI YA KENYA YAANZA KUTEKELEZA MKAKATI KUPUNGUZA MSONGAMANO THIKA SUPERHIGHWAY
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 05, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment