Serikali imepanga kuajiri watumishi
wa kada ya afya wapatao 25,000 katika mwaka wa fedha 2018/19.
Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini
Dodoma leo Jumatatu Aprili 23, na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Josephat Kandege wakati akijibu swali
la Mbunge wa Mbulu Mjini, Zacharia Issay (CCM).
Katika swali la msingi Issay alitaka
kujua serikali ina mkakati gani wa kuongeza watumishi katika Hosptali ya Wilaya
ya Mbulu ambapo Kandege amesema tayari Tamisemi imeomba kibali cha kuajiri
watumishi wa kada ya afya 25,000 ili kuhakikisha kunakuwapo na watumishi wenye
sifa stahiki kwenye hospitali, vituo vyote vya afya na zahanati.
“Serikali inaendelea na ujenzi wa
vituo vya afya 208 nchi nzima ili kuboresha huduna ya dharura kwa mama
wajawazito, ujenzi wa vituo hivyo utagharimu Sh bilioni 132.9 hadi kukamilika.
“Sambamba na ujenzi huo, vituo hivyo
vimetengewa Sh bilioni 35.7 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba ili
kuviwezesha kutoa huduma kwa wagonjwa,” amesema.
Serikali Kumwaga Ajira 25,000 kwa watumishi wa kada ya afya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment