Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano
Tanzania (TCRA) imetaja changamtoto tano za uendeshaji kesi zinazotokana na
makosa ya mtandao.
Changamoto hizo zimetajwa kuwa ni
uelewa mdogo wa majaji, mahakimu na wanasheria, ushahidi wa kuwasilisha,
kufutika kirahisi, uchunguzi, na wapi pa kupeleka malalamiko hayo.
Mwanasheria mwandamizi kutoka TCRA,
Dk Philip Philikunjombe amewataka majaji na mahakimu na wanasheria kupata elimu
juu ya uendeshaji wa kesi hizo kwani kumekuwa na makosa makubwa yanayotendeka.
Mbali na hiyo amesema bado kuna
ugumu wa kujua ni namna gani ushahidi unatakiwa kuwasilishwa mahakamani pindi
mtu atakapokwenda kulalamika kuwa katendewa makosa.
”Umetukanwa kwenye simu je upeleke
simu ya aliyekuwa kwenye simu, je upeleke simu ya aliyekutukana mahakamani,
Tutajuaje kama baada ya kumnyang’anya simu yake hukubadilisha ujumbe. Kama
umechapisha katika karatasi, tutajuaje kama hukuongeza maneno au kupunguza?
Hivyo, bado ni vigumu kupata ushaidi wa kesi hizi” amesema Philikunjombe.
Lakini pia changamoto nyingine ni
ushahidi wa kesi hizo kuharibika kirahisi kwa sababu mtuhumiwa anaweza kufuta
ujumbe hivyo haitakuwa rahisi kuthibitisha makosa hata kama ujumbe huo utakuwa
nao mlalamikaji.
Kufuatia changamoto hizo wadau
mbalimbali wanaotumia mitandao wameshauri wasimamizi wa kesi hizo kupewa elimu
ya sheria zinazohusu makosa ya mtandao ili haki iweze kutendeka.
TCRA yashauri jinsi ya kusuluhisha changamoto kesi za mitandaoni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment