Raisi Magufuli azindua Ukuta

Rais John Magufuli , leo anatarajiwa kuzindua ukuta wa machimbo ya madini ya Tanzanite, uliopo eneo la Mererani mkoani Manyara.
Rais Magufuli aliagiza kujengwa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite mwaka jana ikiwa ni katika kutafuta jitihada za kudhibiti na kuzuia utoroshwaji wa madini hayo, ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee.
Rais Magufuli aliagiza kujengwa kwa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mererani ambapo ukuta huo una urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu.
Pamoja na hayo dhamira nyingine iliyosababisha kujengwa kwa ukuta huo ni kuzuia uhalifu na si kuwazuia wachimbaji wakubwa na wadogo kupata riziki zao.
Ukuta huo umejengwa kwa gharama za Kitanzania isiyozidi bilioni 6.
Raisi Magufuli azindua Ukuta Raisi Magufuli azindua Ukuta Reviewed by KUSAGANEWS on April 06, 2018 Rating: 5

No comments: