Rais John
Magufuli amesema Serikali itaendelea kukopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo,
hata kama kuna watu wanabeza
Amesema fedha
hukopwa kwa masharti nafuu, riba ndogo na hulipwa kwa muda mrefu na kwamba
fedha hizo ndizo hutumika kujenga miundombinu kama barabara ili kuchochea
uchumi
Rais alisema
hayo jana mjini Iringa alipofungua barabara ya lami ya Iringa – Migoli – Fufu
yenye urefu wa kilomita 189 inayounganisha mikoa ya Iringa na Dodoma. Tukio
hilo lilirushwa hewani moja kwa moja na kituo cha televisheni cha TBC 1
Barabara hiyo
iliyojengwa kwa gharama ya Sh207.4 bilioni ni sehemu ya barabara kuu ya kuanzia
Cape Town, Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri.
Imejengwa kwa
ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa asilimia 65.9, Shirika la
Maendeleo la Kimataifa la Japan (Jica) kwa asilimia 21.3 na Serikali ya
Tanzania asilimia 12.8
“Msiwasikilize
wanaosema Serikali ina madeni makubwa wakati wao wenyewe wanapita kwenda
bungeni kwenye barabarani tulizozijenga kwa kukopa,” alisema
Magufuli
alisema Serikali imekuwa ikidaiwa tangu enzi za mkoloni, lakini madeni mengine
yamekuja kulipwa katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete
Akizungumzia
barabara hiyo, Rais alisema inalenga la kuimarisha utalii katika ukanda wa
kusini
“Watu walizoea
(kwamba) ukitaka kutalii ni lazima uende Serengeti wakati Ruaha ni mbuga kubwa
yenye vivutio bora, lakini haikutembelewa na watalii kwa sababu ya ukosefu wa
barabara,” alisema
Kwa sasa
itabidi wenzetu wa kaskazini wasubiri kwanza. Kwa sasa tunaendeleza maeneo
yaliyochelewa kuendelezwa,” alisema
Rais Magufuli
alisema Uwanja wa Ndege wa Nduli uliopo Iringa utaimarishwa ili watalii waweze
kufika maeneo ya utalii
Rais Magufuli
alisema barabara hiyo pia itawasaidia wakazi wa Iringa kusafirisha mazao kwenda
sokoni bila matatizo.
“Barabara hii
iwe mkombozi wa maisha yetu. Tuitunze, itasafirisha mazao, mtasafiri kwa
utulivu kwenda kwenye shughuli zenu,” alisema
Magufuli
ambaye alisoma Shule ya Sekondari Mkwawa mkoani Iringa kuanzia mwaka 1978/79,
alisema anakumbuka hali ya barabara ilivyokuwa tatizo wakati huo
“Kutoka Dodoma
hadi Iringa nilitumia siku mbili kwa kutumia basi la Shirika la Reli Tanzania.
Tulilala njiani kwa sababu ya ubovu wa barabara,” alisema.
Rais Magufuli awajibu wabunge wanaobeza Serikali kukopa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 30, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 30, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment