Katibu wa Itikadi
na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amewataka baadhi ya watu
wanamtuhumu Rais wakidai amelisababishia Taifa hasara kuacha mara moja kwani
hawana uthibitisho wa kauli hiyo.
Polepole amesema hayo kupitia ukurasa
wake wa Twitter, ameandika;
“Ukimtuhumu Rais amelisababishia
hasara Taifa ukaombwa uthibitishe utaweza au utasema yalikuwa tu majadiliano ya
twita baada ya chakula cha mchana?”
“Huko barabarani defamation ni kosa
kubwa, lakini mbona mnataka viongozi wetu wadhalilishwe kisha tukae kimya,
kaanze kumtukana babako” -Polepole.
Defamation ni neno na kosa kisheria
likimaanisha sentensi au tuhuma za uongo ambazo mtu husema au huandika juu ya
mtu mwingine.
Polepole kaanze kumtukana babako
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment