Ndugai amshukuru Mungu kurudi salama

Baada ya kurejea kutoka India alikokuwa akipatiwa matibabu na leo kuongoza kikao cha bunge, Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai amesema anamshukuru Mungu kwa kurudi salama huku akisema wakati alipokuwa kitandani kuna wakati alikuwa akiona kama hapakuchi.
Akielezea hali yake leo Bungeni kwa mara ya kwamba Sopika Ndugai amesema kwamba hawaombei Wabunge wapitie katika hali aliyoipitia bali anawaombea wasipitie machungu ambayo yeye yalimpata.

Spika Ndugai amesema kwamba " Baadhi yenu labda hamjawahi kulazwa hospitali mkiwa mnaumwa sanaa halafu somehow ukawa pekee yako unaweza kuona Kuna wakati fulani mawazo yanavyokuja yanavyozunguka na wakati mwingine  dalili zilikuwa zinataka kuonyesha kama kesho kunaweza kusikuche hivi... ina raha yake na tabu yake kidogo. Siwaombei mpitie katika mambo hayo nawaombea msipate machungu hayo".

Mbali na hayo Ndugai amewapongeza wasaidizi wake wakiongozwa na Naibu Spika Ackson Tulia na Katibu wake pamoja na wabunge wote kwa ujumla na kuwaomba waendeleze gurudumu kwani kipindi kinachofuata ni kirefu sana cha Bunge la Bajeti.

Pamoja na hayo amewashukuru sana wale wote waliomuombea na kumjulia hali alipokuwa kwenye matibabu hususani Waziri mkuu Kassim Majaliwa, aliyekuwa akimjulia hali mara kwa mara pamoja na Wananchi wa jimbo lake (Kongwa).
Ndugai amshukuru Mungu kurudi salama Ndugai amshukuru Mungu kurudi salama Reviewed by KUSAGANEWS on April 09, 2018 Rating: 5

No comments: