Kuhojiwa Uhamiaji siyo suala la Kisiasa


Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Crispin Ngonyani amesema kuwa suala la wao kuwaita watu mbalimbali katika ofisi zao hakuna mahusiano na  mashinikizo ya kisiasa na kuongeza kwamba wana uwezo wa kumhoji mtu yoyote ambaye watakuwa na mashaka naye.
Akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kumhoji  Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe, Ngonyani amesema kwamba yeye hapelekeshwi kisiasa bali anafanya kazi kitaalamu kutokana na sheria inavyomtuma.

Ameongeza kwa mujibu wa sheria ya uraia ana uwezo wa kumsimamisha mtu yoyote na kumhoji swali la uraia au kuhusu suala la uhamiaji kama ni mgeni na kujibiwa kwa ufasaha.

"Sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria siyo kwa shinikizo la kisisasa hata kidodo. Na ndiyo maana mmemuona anatoka hapa akiwa anatabasamu. Hata yule Nondo alikuja tukamhoji maswala ya kiuhamiaji na siyo kisiasa na akatoka hapa akiwa anatabasamu kabisa. Mtu anaweza akaja hapa ana mawazo 100 lakini akitoka ana tabasamu. Nafikiri mmemuona Askofu" Ngonyani amesema.

Kwa upande wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amefunguka baada ya kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani katika Idara ya Uhamiaji na kusema kuwa watu hao wamemuhoji kuhusu uraia wake na kudai kuwa wamechukua passport yake. 

Mchungaji Kakobe amedai kuwa watu hao hata kipindi cha nyuma walishakwenda kuchunguza juu ya uraia wake kwa kuwauliza ndugu na jamaa mbalimbali na kujiridhisha kuwa yeye ni raia wa Tanzania hivyo anadai anashangwaza kuona akiitwa sasa tena kwa ajili ya suala la uraia. 
Kuhojiwa Uhamiaji siyo suala la Kisiasa Kuhojiwa Uhamiaji siyo suala la Kisiasa Reviewed by KUSAGANEWS on April 09, 2018 Rating: 5

No comments: