Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles
Tizeba amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Methew Mtigumwe,
kusitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndg. Hassan
Jarufo.
Waziri Tizeba ametoa agizo hilo kwa
katibu mkuu wa wizara hiyo jana jioni wakati leo akizungumza na wanahabari
ofisini kwake mjini Dodoma ikiwa ni muda mchache mara baada ya kumalizika kwa
hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa maghala na vihenge vya
kisasa.
Mhe. Dkt Tizeba amesema uamzi wa
kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo, umekuja baada ya kuangalia mwenendo wa
Ndg. Jarufo na kutafakari jinsi zao la Korosho linavyoendeshwa, ikiwa ni pamoja
na kutoridhishwa na upatikanaji wa viuwatilifu kwa wakati.
Mkataba wa Jarufo umesitishwa
kuanzia Aprili 21 na kwa mujibu wa Waziri Tizeba alisema ndani ya muda
mfupi Wizara ya kilimo itamtangaza Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo ili kuchukua
nafasi hiyo na kuendeleza kusimamia sekta hiyo.
Aidha Mh. Tizeba ameongeza kuwa
hatua kama hizo serikali inazichukua lengo ikiwa ni kuhakikisha kuwa
wadau wakubwa wa Korosho ambao ni wakulima wanaendelea kunufaika na zao hilo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho atumbuliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment