Kufuatia mdogo wake Mange Kimambi kufika Ofisini kwa Mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro wake wa kutelekeza mtoto
Mange amesema kuwa hajafurahishwa na kitendo hicho.
Amesema kuwa amechukizwa na kitendo hicho cha mdogo wake kufika
ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, ambapo ameandika
kwenye ukurasa wake Instagram ataifufua kesi ya mirathi iliyoamuliwa mwaka
2016.
Aidha, katika hatua nyingine Mange ameituhumu familia yake kwa
kuuza machimbo ya urithi ya kokoto kwa bei ndogo yaliyopo Tegeta jijini Dar es
salaam bila kupewa taarifa wala kutumiwa mgao wake.
“Nilikuwa tayari niishi vibaya ila nyinyi muishi vizuri ndio maana
sikuwasumbua na mali za baba yetu, Mgao wangu wa machimbo ya kokoto mliyouza
muanze kunitafutia. Mlidhani sijui? Kweli mnadhani sijapewa habari za nyinyi
kuuza machimbo yetu ya kokoto? Nilikuwa najua Ila niliamuwa kukaa kimya sababu
nawapenda na bila nyinyi kwenye maisha yangu nahisigi siwezi kuishi ila labda
nahitaji kujifunza kuishi bila nyinyi,”ameandika Mange kwenye ukurasa wake wa
Instagram
Hata hivyo, amesema kuwa mpaka sasa hajachukua chake kwani hadi
leo ni miaka 12 sasa imepita tangu jaji awagawanye mali za urithi
Mange Kimambi kuwaburuza mahakamani ndugu zake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment