Makonda asema hawezi kufanya maongezi ya Siri na wanaume waliotelekeza watoto

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameweka wazi kuwa hayupo tayari kufanya maongezi ya chemba na wanaume waliotelekeza watoto wao kwa madai kuwa wanaona aibu kufika ofisini kwake.
Akizungumza leo na wananchi waliojitokeza katika ofisi yake kutafuta msaada wa kisheria baada ya kutelekezewa watoto na wenzi wao, Makonda amesema hatakuwa tayari  wala kuwa na muda wa kumsikiliza mwanaume aliyemtelekeza mwanamke na mtoto na kwamba kwa sasa yupo kusaidia wapate haki zao.

Aidha amesema kwamba kati ya wazazi waliofika ofisini kwake amegundua wapo watu wa makundi tofauti tofauti waliofika ofisini kwake ambapo kundi la kwanza ameshukuru na analipongeza kwa kuwa wameamua kumaliza tofauti zao baada ya kusikia mambo yamefika kwake.

Mbali na hayo Makonda amesema wale watu wanaolalamika mitandaoni kwa kudai kuwa kulitakiwa kufanyike kwa usiri wa jambo hilo, wanapaswa kutoa huduma kwa watoto wao ili wasiabishwe hadharani.

Aidha ameweka wazi kwamba mpaka sasa mezani kwake yapo majina ya watu mashuhuri  107 ambao nao wametajwa kutelekeza watoto wao.
Makonda asema hawezi kufanya maongezi ya Siri na wanaume waliotelekeza watoto Makonda asema hawezi kufanya maongezi ya Siri na wanaume waliotelekeza watoto Reviewed by KUSAGANEWS on April 11, 2018 Rating: 5

No comments: