Kontena Lauwa Mtu Mmoja

Gari kubwa lenye kontena limeanguka kwenye eneo la Ubungo external na kuua mtu mmoja, ambaye inasadikiwa alikuwa abiria kwenye gari hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo wakati dereva wa gari hilo akijaribu kulikwepa gari dogo na kuanguka.
Kamanda Muliro amesema mazingira ya ajali mpaka sasa hajayaeleweka, kwani dereva wa gari amekimbia na hawajampata.
Kamanda Muliro ameendelea kwa kusema kwamba wamefanikiwa kulitoa kontena hilo na kutoa mwili wa marehemu, lakini mpaka sasa wanashindwa kuelewa kama mtu huyo alikuwa kwenye gari au alikuwa nje, kulingana na mazingira ya tukio na taarifa walizopata.

Kontena Lauwa Mtu Mmoja Kontena Lauwa Mtu Mmoja Reviewed by KUSAGANEWS on April 11, 2018 Rating: 5

No comments: