Hawa hapa waliopandishwa vyeo na JPM leo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo Aprili 12, 2018 amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika vyeo mbalimbali na kumteua Kanali Bernard Masala Mlunga kuwa Mpambe wa Rais (Aide de Camp – ADC).

Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Paul Massao kuwa Luteni Jenerali.

Meja Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli (TMA) na kwa uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa na Luteni Jenerali wawili.

Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Brigedia Jenerali Henry Kamunde kuwa Meja Jenerali.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 27 wa JWTZ kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali na Afisa 1 kutoka Luteni Kanali na kuwa Kanali.

Kwa taarifa kamili soma hapa chini..

Hawa hapa waliopandishwa vyeo na JPM leo Hawa hapa waliopandishwa vyeo na JPM leo Reviewed by KUSAGANEWS on April 12, 2018 Rating: 5

No comments: