Kocha wa
zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson leo amemuaga kocha wa Arsenal
Arsene Wenger kwa kumpa zawadi maalum kabla ya mechi ya ligi kuu iliyomalizika
kwa kufungwa 2-1 usiku huu kuanza.
Fergusona
amemkabidhi zawadi hiyo kwaniaba ya klabu ya Manchester United ikiwa ni sehemu
ya kutambua mambo mbalimbali ambayo Wenger ameyafanya kwenye ligi kuu ya soka
ya England EPL.Wenger
ametangaza rasmi kuachana na Arsenal aliyoifundisha kwa miaka 22 mwishoni mwa
msimu huu. Hata hivyo Wenger bado hajaweka wazi kama atastaafu au atakwenda
kufundisha timu nyingine.
Katika
mchezo uliopigwa jioni hii kwenye uwanja wa Old Trafford, Wenger ameshinwa
kulinda heshima ya kutofunga baada ya vijana wake kuruhusu bao la dakika za
mwisho kutoka kwa Marouane Fellaini.
Mabao ya
Man United yamefungwa dakika ya 16 na kiungo Paul Pogba na dakika ya 90 na
Marouane Fellaini huku lile la Arsenal likifungwa na Henrikh Mikhtaryan dakika
ya 51. Wenger na Mourinho sasa wamekutana mara 13 na Mourinho ameshinda mara 8
na kutoka sare mara 5.
Ferguson ampa zawadi Wenger, aaga kwa kipigo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 30, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment