Katibu wa Halmashauri
Kuu Itikadi na Uenezi ya CCM, Humphrey PolePole amefunguka na kusema kuwa wao
kama Chama Cha Mapinduzi na serikali hakuna mtu kati yao aliyemjibu Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad bali CHADEMA ndiyo
wamemjibu.
Polepole amesema hayo leo April 22,
2018 kupitia mtandao wake wa twitter na kudai kuwa wao waliipokea ripoti hiyo
na kumpongeza CAG na kuitaka serikali iendelee kuchukua hatua katika yale
ambayo CAG ameyabaini.
"Kimsingi kwa CCM au Serikali
yake hakuna hata mtu mmoja ambaye amemjibu CAG, sisi tulipokea, tulipongeza na
tukaelekeza Serikali iendelee kuchukua hatua. Ambaye amejitokeza kujibu
hadharani ni CHADEMA ndio pekee wamemjibu na kumkosoa CAG. Ila naona watu
wachache pamba masikioni" alisisitiza
Polepole
Polepole anasema yeye alipowaita
waandishi wa habari hakumjibu CAG bali amedai kuwa alifanya ufafanuzi wa hoja
mbalimbali ikiwepo ile ya Trilioni 1.5 ambayo kwenye ruipoti ya CAG inaonekana
haina maelezo.
"Kuna tofauti kati ya kumjibu
CAG na kufafanua hoja ambazo amezitoa kwa CCM na kuulaani vikali upotoshaji wa
Zitto Kabwe juu ya taarifa ya CAG"
CHADEMA ndiyo wamemkosoa CAG - Polepole
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment