CCM yaja juu viongozi wa upinzani wanaodaiwa kupotosha ripoti ya CAG

Chama cha Mapinduzi(CCM) kimesema kuwa kuna viongozi wa upinzani wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kuupotosha umma, tabia ambayo haikubaliki, haivumiliki na itafika wakati watasema sheria ichukue mkondo wake maana wanaleta taharuki kwa wananchi

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole amesema hayo leo Jumatano Aprili 18 wakati akifafanua mambo kadhaa yanayopotoshwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG

Polepole amesema imekuwa tabia na mtaji wa kiongozi huyo ambaye hakumtaja jina kutoa taarifa za uongo

“Kiongozi unasema fedha zimeibiwa sijiu akiambiwa atoe ushahidi atasemaje. Siku hizi hana hoja ana kazi ya kuleta taharuki kwa umma,” amesema Polepole
“Hatuko tayari kuendelea kuona watu wachache wauhadaa umma.”
Amesema CCM hakiamini malumbano, mabishano yasiyo na tija, lugha za kubeza, kebehi na kufifisha moyo wa kizalendo kwa Watanzania
“Nchi yetu ina mfumo wa kidemokrasia ya vyama vingi lakini CCM inaendelea kuamini sisi ni wamoja.”
CCM yaja juu viongozi wa upinzani wanaodaiwa kupotosha ripoti ya CAG CCM yaja juu viongozi wa upinzani wanaodaiwa kupotosha ripoti ya CAG Reviewed by KUSAGANEWS on April 18, 2018 Rating: 5

No comments: