BEI YA PETROLI, MAFUTA TAA YASHUKA HUKU DIZELI IKISALIA PALE PALE


BEI ya mafuta taa na petroli nchini Kenya imeshuka na sasa yatauzwa Sh76.72 na Sh106.83 mtawalia kwa lita moja jijini Nairobi katika kipindi cha mwezi mmoja ujao kati ya Aprili 15, 2018, hadi Mei 14, 2018.

Bei hiyo imeshuka kwa Sh0.73 kutoka ile ya awali ya Sh77.45 kwa mujibu wa bei mpya zilizotolewa jana na Tume ya Kudhibiti Kawi (ERC).

atika taarifa hiyo, bei ya petroli pia imepungua kwa Sh0.46 na sasa lita moja itauzwa Sh106.83 Nairobi ikilinganishwa na Sh107.46 kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Hata hivyo, bei ya dizeli inasalia kama ilivyokuwa ikiuzwa mwezi kipindi ambacho kimepita– Sh97.86 kwa lita.

Bei hizo mpya zimetangazwa na Tume ya Kudhibiti Kawi (ERC).
Mabadiliko hayo yametokana na kupungua shuka kwa ada iliyotozwa bidhaa za mafuta zilipotua nchini kutoka soko la kimataifa.

Wakazi wa Pwani katika Kaunti ya Mombasa, ambako shehena ya bidhaa hizo hutua bandarini, watanunua lita moja ya mafuta taa kwa Sh73.94 ikilinganishwa na Sh74.68 mwezi jana.

Wenye magari madogo watanunua petroli Sh103.54 huku madereva wa malori na mabasi pamoja na kampuni za kuunda bidhaa ambazo huhitaji dizeli kuendesha mashine zikinunua lita moja ya dizeli kwa Sh94.57.

Wateja mjini Nakuru watanunua mafuta taa Sh77.56, petroli Sh107.53 na dizeli Sh98.76 kwa lita kuzingatia gharama ya usafirishaji ambazo wafanyabiashara hukutoka bandarini.

Bei mjini Eldoret itakuwa Sh78.63 kwa kila lita ya mafuta taa ikilinganishwa na Sh79.36 mwezi jana. Petroli itakuwa Sh108.71 ikilinganishwa na Sh109.33 mwezi uliopita huku dizeli ikisalia Sh99.94.

Katika Kaunti ya Kisumu wenyeji watanunua mafuta taa Sh78.62, petroli Sh108.78 na dizeli Sh100.01.

Wakazi katika mji ulio mbali zaidi wa Isebania watanunua mafuta taa Sh80.71, petroli Sh110.86 na dizeli Sh102.09.

BEI YA PETROLI, MAFUTA TAA YASHUKA HUKU DIZELI IKISALIA PALE PALE BEI YA PETROLI, MAFUTA TAA YASHUKA HUKU DIZELI IKISALIA PALE PALE Reviewed by KUSAGANEWS on April 15, 2018 Rating: 5

No comments: