Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara
linawashikilia wanafunzi 9 wa Chuo Kikuu cha Stella Maris na Daktari mmoja wa
Hospitali ya Mission Nanyamba kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kupitia
mitandao ya kijamii ya WhatsApp na Telegram.
Hatua ya kuwashikilia watu hao ni
kufuatia agizo la Rais JPM la kukemea vikali watu wa namna hiyo wanaohamasisha
maandamano huku akidai kuwa Tanzania ni nchi ya amani, hivyo maandamano
hayaruhusiwi kufanyika..
“Wapo watu wangependa nchi hii kila
siku tuwe na migogoro, Wapo watu ambao wameshindwa kufanya siasa za kweli,
wangependa kila siku tuko barabarani tunaandamana. Watu wao wanahamia huku, wao
wanataka wabaki wanaandamana kule.
Nitasema ngoja waandamane wataniona. Kama
kuna baba zao wanawatuma, watakwenda kuwasimulia vizuri.
Niliapa kwa katiba
kwamba nchi hii lazima iwe ya amani.” Amesema Rais John Pombe Magufuli.
Rais alizungumza hayo mnamo mwezi
Machi mwaka huu pindi akijaribu kukemea harakati za maandamano zinazoendelea
nchini, ambapo inadaiwa kuwa kuna watu wasiojulikana wanahamasisha kufanyika
kwa maandamano Aprili mwaka huu.
10 Watiwa mbaroni kwa kuhamasisha maandamano
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment