WAZIRI wa Fedha na
Mipango,Dk. Philip Mpango amepiga marufuku kwa shirika lolote kufanya makadirio
ya idadi ya watu wa Tanzania na kuchapisha matokeo hayo bila kushirikisha Ofisi
ya Taifa ya Takwimu na atakayebainika kufanya hivyo watamchukulia hatua kali za
kisheria.
Dk.Mpango amesema hayo
jana jijini Dar es Salaam wakati anazindua taarifa ya makisio ya idadi ya watu
Tanzania ambapo alisema kwa makadirio yaliyotokana na Sensa ya Watu na Makazi
ya mwaka 2012.
Viwango vya uzazi na
vifo kwa takwimu za mwaka 2016, idadi ya watu Tanzania sasa ni milioni
54.2 ambapo Tanzania Bara ni watu milioni 52.6 na
Tanzania Bara watu milioni 1.6 kwa mwaka 2018.
Dk.Mpango aliisema
idadi hiyo inakadiriwa kufikia watu milioni 59.4 mwaka 2021 na ifikapo mwaka
2030 idadi ya watu itafikia milioni 77.5.
Pia Dk.Mpango
aliwakumbusha wadau wote wa ndani na nje ya nchi kuwa takwimu za idadi ya watu
kwa nchi ya Tanzania ni hizo ambazo amezitangaza jana na si vinginevyo.
Alifafanua kwa
kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 inakadiriwa kuwa
kila mwaka kuna ongezeko la wastani watu wapatao milioni 1.6 hapa nchini.
Dk.Mpango alisema
ongezeko hill linatokana na idadi kubwa vya vizazi vipatavyo milioni 2.0
ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo ambavyo ni takribani 400,000 kwa mwaka.
“Utafiti wa mama na
mtoto wa mwaka 2015/16 unaonesha kwamba mwanamke wa kitanzania atazaa watoto
watano katika maisha yake yote ya uzazi .
” Hata hivyo kiwango
cha uzazi kilipungua kutoka wastani wa watoto 7 mwaka 1978 had I wastani wa
watoto watano mwaka 2016.Baadhi ya sababu za juu cha uzazi ni kiwango kikubwa
cha vifo vya watoto,familia kupendelea kuwa na watoto
wengi,umasikini,mila,imani za kidini na matumizi madogo ya uzazi wa
Mpango,”alisema.
Aliongeza matokeo yake
ni kuwa na idadi ya watu hapa nchini imeendelea kuongezeka na kuifanya Tanzania
kuwa nchi ya sita katika Bara la Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu baada
ya Nigeria, Ethiopia, DRC na Misri.
Alisema kwa mtazamo
wake wingi au au uchache wa idadi ya watu sio tatizo bali tatizo ni pale ambapo
kasi ya ongezeko la idadi hiyo inazidi kasi ya ukuaji wa uchumi na hivyo
kulifanya Taifa kushindwa kumudu ipasavyo mahitaji ya wananchi.
Dk.Mpango alisema kasi
ya ongezeko la idadi ya watu pia inaleta changamoto ya idadi kubwa ya watoto na
vijana .”Kwa mfano takwimu nilizozizindua leo zinaonesha asilimia 50 ya watu
wote nchini ni watoto wenye umri chini ya miaka 18.
“Asilimia hii kubwa ya
watoto katika nchi zinazoendelea inatokana na mabadiliko ya kidemografia kutoka
viwango vya juu vya vifo lakini wakati huo viwango vya uzazi vibaki juu,”
alisema.
Aliongeza asilimia
kubwa ya watoto ni changamoto kwa maendeleo ya nchi yoyote duniani kwa vile
kundi hilo lina mahitaji ya kipekee ambayo lazima yatimizwe na Serikali na
jamii kwa ujumla wake.
Dk.Mpango alisema
mojawapo ya changamoto hizo ni kiwango cha juu cha utegemezi kinachotokana na
idadi kubwa ya watoto.
Alisema kwa mfano kwa
mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kiwango cha utegemezi
kiumri ni asilimia 92 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 40 kwa nchi
zinazoendelea.
Hiyo ikiwa na maana
kuwa kwa Tanzania kila watu 100 wenye umri wa miaka 15 hadi 64 wanategemewa na
watu 92 wenye umri chini ya miaka 15 wenye umri zaidi ya miaka 65.
WAZIRI MPANGO APIGA MARUFUKU MASHIRIKA YANAYOFANYA MAKADIRIO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment