WAZIRI wa TAMISEMI, Suleman Jafo, amewapa mwezi mmoja
makatibu tawala mikoa kuhakikisha wanapeleka taarifa za mabaraza mangapi ya
walemavu yaliyoundwa kuanzia ngazi ya kata, wilaya na mkoa yatakayoshughulikia
masuala yao hususan elimu.
Jafo alisema hayo
jana wilayani Kisarawe alipokuwa akipokea msaada wa vifaa vya watu wenye
ulemavu vilivyotolewa na shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masula
ya watu wenye ulemavu la ADD International.
“Tumeshatoa waraka na sasa tunataka utekelezaji, tu kabla ya Aprili 30 nipate taarifa ni mabaraza mangapi yameundwa kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa na yasiundwe kama komedi, bali yahakikishe yanashughulikia masuala ya watu wenye ulemavu,” alisema.
Alipongeza Wilaya ya Kisarawe kuwa ya kwanza kuunda baraza la watu wenye ulemavu, baada ya waraka huo kutolewa na ofisi yake, na kusisitiza kuwa mabaraza hayo ni muhimu katika ustawi wa watu wenye ulemavu hasa katika kusimamia elimu.
Katika hatua nyingine, Jafo amemwagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Kisarawe, Wanchoke Chinchibera, kuhakikisha wanajenga choo cha mtoto mwenye ulemavu wa miguu wa darasa la tano Shule ya Msingi Kazimzumbwi, Yusufu Kondo (14), baada ya mtoto huyo kueleza changamoto zinazomkwamisha kielimu, ikiwamo kukosa choo rafiki kutokana na ulemavu.
“Naagiza choo kijengwe hadi kufikia Ijumaa kiwe kimekamilika, kama mtakwama mnieleze niwasaidie na mtoe taarifa mapema kabla, tumejenga shule, zahanati na miradi mingine mingi,” alisema na kuongeza:
“Choo kwa ajili ya huyu mwanafunzi na wengine wenye ulemavu kama wake hakitatushinda, tutakijenga ili mtoto huyu asome vizuri na kufikia ndoto zake.”
Pia aliagiza maofisa ustawi wa jamii na maendeleo katika halmashauri zote kuhakikisha wanawatambua watoto wenye ulemavu na kubainisha changamoto zao za msingi na kuzipatia ufumbuzi ikiwamo kuwawezesha ili kupata elimu kwa kuwa Serikali inatoa kila mwezi Sh. milioni 23 .8 kwa ajili ya watoto wenye ulemavu kupata elimu katika mazingira rafiki.
Msaada huo wa vifaa vya watu wenye ulemavu umegharimu Sh. 174, 577, 000 na ulitolewa na Mkurugenzi wa ADD International, Rose John, kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu walioko mashuleni katika shule 12 za wilaya za Kisarawe, Mkuranga , Kibaha Mjini na Kibaha Vijijini.

Waziri Jafo ataka Mabaraza ya Walemavu kuundwa kuanzia ngazi ya Kata
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment